Shilingi ya Kenya yazidi kuimarika wa thabiti dhidi ya dola, kuuzwa kwa Sh145 na nunuliwa 148 mtawalia - Benki za Kenya zasema

Mwenyekiti wa muungano wa benki nchini (KBA) John Gachora alisema hii inachangiwa na kukua kwa imani katika utendaji na mtazamo wa uchumi wa Kenya.

Muhtasari

• KBA imesema kuwa kuimarika kwa dola kunachangiwa na kukua kwa imani katika utendaji na mtazamo wa uchumi mkuu wa Kenya.

PESA ZA KENYA
PESA ZA KENYA
Image: STAR

Muungano wa Mabenki wa Kenya (KBA) umebaini kuwa Shilingi ya Kenya imeimarika pakubwa dhidi ya dola ya Marekani.

Chama cha Mabenki cha Kenya (KBA) ndicho kikundi kikuu cha utetezi katika sekta ya fedha na chombo mwavuli cha taasisi zilizopewa leseni na kudhibitiwa na Benki Kuu ya Kenya (CBK) chenye uanachama wa wa taasisi 46 za kifedha.

Mwenyekiti wa KBA ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NCBA John Gachora alisema kufikia Alhamisi jioni, soko lilifunga viwango vya kununua na kuuza vilivyochapishwa kwa bei ya wastani ya Sh145 na Sh148 mtawalia.

Alisema kiasi hicho kinaonyesha faida kubwa kutoka kwa safu za hivi karibuni za biashara.

"Ikizingatiwa kuwa Kenya ilikomboa akaunti yake ya mtaji katika miaka ya 1990, kiwango cha ubadilishaji kinatarajiwa kuelekea upande wowote ili kuakisi nguvu za usambazaji na mahitaji wakati wowote," alisema katika taarifa.

Gachora aliongeza kuwa kuimarika kwa dola kunachangiwa na kukua kwa imani katika utendaji na mtazamo wa uchumi mkuu wa Kenya.

Alisema kuwa ni pamoja na mafanikio ya ombi la Eurobond ya Dola 1.5 (Sh238 bilioni) na kufanikisha utoaji wa Eurobond ya miaka 8.5. ya miundombinu.

Kulingana na KBA, Data kutoka Benki Kuu ya Kenya inathibitisha kwamba tulipokea Eurobond ya jumla ya thamani ya shilingi 288 bilioni, na Benki Kuu (CBK) ilikubali tu shilingi bilioni 240.9.

Alisema dhamana ya miundombinu (Infrastructure bond ) ilileta hamu kubwa ya wawekezaji kutoka nje, hivyo kusababisha uthabiti wa shilingi kama ilivyotarajiwa.

KBA iliipongeza zaidi serikali na CBK kwa usimamizi wao wa kiuchumi wakati wa misukosuko katika historia ya uchumi wa nchi.