Whozu: Wanaomtongoza Wema Sepetu DM wanachati na mimi

Akichagiza mkwara wake Zaidi, Whozu alisema kwamba kwa wale ambao wanatanua vifua kuwa Wema Sepetu amewajibu inbox, basi wajue kwamba si Wema aliwajibu bali ni yeye

Muhtasari

• "Wakiamua kustop na mimi nitastop. Na tukikutana kwenye sehemu tofauti tutaendelea kucheka,” alisema 

Image: INSTAGRAM// WHOZU

Msanii Whozu ametoa mkwara mzito kwa vidume wanaomtongoza mpenzi wake Wema Sepetu kupitia faragha za akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Akizungumza na blogu ya Simulizi na Sauti ya nchini Tanzania, Whozu alisema kwamba yeye ana uthibiti wa akaunti za Wema na anaona kila ujumbe unaoingia.

Akichagiza mkwara wake Zaidi, Whozu alisema kwamba kwa wale ambao wanatanua vifua kuwa Wema Sepetu amewajibu inbox, basi wajue kwamba si Wema aliwajibu bali ni yeye mwenyewe ndiye aliwajibu.

“Na ninawashauri, kama mtaendelea basi tutaendelea kuchati, msifikirie mnachati na mama [Wema], mimi naziona na mimi ndio nazijibu jumbe zenu. Wakiamua kustop na mimi nitastop. Na tukikutana kwenye sehemu tofauti tutaendelea kucheka,” alisema kwa madoido.

Whozu alisema kwamba anawajibu jinsi wanavyokuja, kwa maana kwamba mwanamume akianza kumtumia jumbe Wema kwa kumutamkia neno la kimahaba na yeye huwajibu vile vile kwa kutumia maneno ya kimahaba.

Awali, Whozu alifunguka kwamba bado Imani yake inamtuma kuamini kuwa ipo siku yeye na Wema watapata mtoto wao pamoja, licha ya watu kudai kwamba Wema hana uwezo wa kubeba ujauzito tena.

Whozu alisema kwamba anaamini atakuja kuitwa baba na binti wa pili kutoka kwa uzao wa Wema.