Bado naamini ipo siku nitazaa mtoto na Wema Sepetu - Whozu

Whozu alifichua kwamba yeye anaona akipata mtoto wa kike na Wema japo kwa upande wa Wema, ndoto yake ni kupata mtoto wa kiume.

Muhtasari

• “Ninachoamini mimi na wewe tutaenda mpaka tupate mtoto mwingine ambaye atakuwa mdogo wake Lola," alisema.

Wema Sepetu ni mjamzito, Whozu afichua.
Wema Sepetu ni mjamzito, Whozu afichua.
Image: Instagram

Msanii na muigizaji Whozu amejitokeza kimasomaso kumtetea mpenzi Wake Wema Sepetu dhidi ya madai ya watu kwamba hazai.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Whozu alisema kwamba yeye na mpenzi wake wameshayazoea ya watu, akiwema wazi kwamba Imani yake bado ipo pale pale kwamba siku moja watabarikiwa na mtoto pamoja.

Whozu alisema kwamba hajali wala kusikiliza maneno ya watu na kile anachoamini ni kwamba Wema Sepetu atamzalia mtoto.

“Mimi wala sifuati uzungu na ninamini ipo siku nitazaa na Wema. Imani yangu bado inaniambia kwamba Mwenyezi Mungu atatubariki tutapata mtoto. Kwa hiyo ninamwambia kila siku kwamba usihofu, hutakiwi kuwaza sana, hutakiwi kuwaza vibaya wala kuona kwamba ndio ushamaliza. Hapana,” Whozu alisema.

Msanii huyo alisema kila siku anampa msukumo na hamasa Wema Sepetu kwamba katika maisha yake bado anamuona mtoto wake wa pili akitokea katika tumbo lake.

“Ninachoamini mimi na wewe tutaenda mpaka tupate mtoto mwingine ambaye atakuwa mdogo wake Lola, na mtoto wetu atakuwa anamuita mdogo wake Lola aje akae na yeye,” alisema.

Whozu alifichua kwamba yeye anaona akipata mtoto wa kike na Wema japo kwa upande wa Wema, ndoto yake ni kupata mtoto wa kiume.