Mahakama ya Rwanda yamzuia kiongozi wa upinzani kuwania urais

Victoire Ingabire alisema kwamba mahakama ya Rwanda "iko mbali na uhuru" ikiwa katiba ilimpa haki, "lakini jaji aliegemeza kwa amri ya rais.

Muhtasari

• Kiongozi huyo wa upinzani Victoire Ingabire alikuwa mehukumiwa miaka 15 lakini alisamehewa na Kagame baada ya miaka minane gerezani.

• Bi Ingabire alitarajia kushindana na rais katika uchaguzi ujao.

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire.
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire.
Image: BBC

Mahakama kuu katika mji mkuu wa Rwanda Kigali imetupilia mbali ombi la kiongozi maarufu Victoire Ingabire kutaka kurejeshewa haki zake zote za uraia ambazo zitamruhusu kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi Julai.

Bi Ingabire aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama kwamba mahakama ya Rwanda "iko mbali na uhuru" ikiwa sheria ya juu (katiba) ilimpa haki, "lakini jaji leo aliegemeza uamuzi wake juu ya amri ya rais".

Bi Ingabire ambaye amefungwa kwa miaka minane na kusamehewa na Rais Paul Kagame mwaka 2018 kabla ya kukamilisha kifungo chake cha miaka 15, alitarajia kushindana na rais katika uchaguzi ujao.

"Sikubaliani na kile jaji alisema, na kwa bahati mbaya huwezi kukata rufaa kabla ya miaka miwili ... Bado tuko mbali na nchi inayotii sheria" aliwaambia waandishi wa habari.