Tanzania na Uenyekiti wa AU: Ikifika wakati muafaka tutasema- January Makamba

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania January Makamba alisema Tanzania itatoa kauli yake wakati muafaka.

Muhtasari

• Waziri Makamba alithibitisha kuwa mazungumzo bado yanaendelea miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Image: MAKTABA

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba amesema kuwa mashauriano katika ukanda wa Afrika mashariki juu ya uenyekiti wa umoja wa Afrika unaendelea na ikifika wakati muafaka Tanzania itatoa kauli yake.

Makamba ameyesema hayo wakati wa mazungumzo maalum na mwandishi wa BBC Leornad Mubali.