Ujumbe wa Mudavadi kwa Iran kufuatia kifo cha Rais Raisi katika ajali ya chopa

Ameongeza kuwa "akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, Abdollahian alichangia pakubwa sio tu katika kukuza amani, usalama na utulivu wa kikanda

Muhtasari
  • Katika ujumbe kwa Ali Bagheri, naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Iran, Mudavadi pia amemuomboleza mwenzake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, aliyeangamia pamoja na Rais Raisi na watu wengine saba.
Musalia Mudavadi
Musalia Mudavadi
Image: Facebook

Waziri wa Mashauri ya Kigeni Musalia Mudavadi amemuomboleza marehemu Rais wa Iran Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ya ndege Jumapili jioni.

Katika ujumbe kwa Ali Bagheri, naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Iran, Mudavadi pia amemuomboleza mwenzake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, aliyeangamia pamoja na Rais Raisi na watu wengine saba.

"Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Kenya, wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora ya Jamhuri ya Kenya, na kwa niaba yangu binafsi, ningependa kuwasilisha rambirambi zangu nyingi kwa Mheshimiwa na, kupitia kwako, kwa familia na marafiki wa walioaga dunia, na kwa watu wa Iran,” Mudavadi alisema.

Ameongeza kuwa "akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, Abdollahian alichangia pakubwa sio tu katika kukuza amani, usalama na utulivu wa kikanda, lakini pia aliwekeza nguvu zake katika kuimarisha uhusiano kati ya Iran na mataifa yake rafiki, kama vile Kenya."

"Atakumbukwa daima kwa kujitolea kwake bila kuchoka na kujitolea kwa wananchi wenzake na kwa nia ya Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," Mudavadi alimpongeza mwenzake.