Ruto afurahia kukutana na nguli wa ‘NBA’ Shaquille O'Neal nchini Marekani

Rais alikutana na O'Neal wakati wa ziara yake katika bustani ya Kitaifa ya Kihistoria ya Martin Luther King Jnr huko Atlanta.

Muhtasari

• Rais alikutana na O'Neal wakati wa ziara yake katika bustani ya Kitaifa ya Kihistoria ya Martin Luther King Jnr huko Atlanta.

Rais William Ruto, balozi Meg Whitman wote wakitabasamu walipokutana na nguli wa NBA Shaquille O'Neal nchini Marekani Jumanne, Mei 21, 2024.
Rais William Ruto, balozi Meg Whitman wote wakitabasamu walipokutana na nguli wa NBA Shaquille O'Neal nchini Marekani Jumanne, Mei 21, 2024.

Rais William Ruto alikuwa mwenye furaha siku ya Jumanne alipokutana na nguli wa mpya wa kikapu nchini Marekani Shaquille O'Neal.

Rais alikutana na O'Neal wakati wa ziara yake katika bustani ya Kitaifa ya Kihistoria ya Martin Luther King Jnr huko Atlanta.

Katika video, Rais alishangazwa sana na urefu wa gwiji huyo wa NBA ambaye kimo chake kiliwadumaza watu wengine waliokuwepo.

Aliushika mkono wa O'Neal kwa furaha huku akiweka mkono wake mwingine kwenye bega la machezaji huyo was awali. akionekana kupigwa na butwaa kwa urefu wake.

Rais aliendelea kumtazama bingwa huyo wa zamani wa NBA walipokuwa wakipiga gumzo.

Wakati wa mkutano huo Rais Ruto alikuwa ameandamana na mkewe, Mama Rachel Ruto na Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman.

IMETAFSRIWA NA DAVIS OJIAMBO.