Mzee wa miaka 52 afariki akirusha roho na kipusa wa miaka 24 kwenye lodging

Mwili wa Naftali Nyadera ,52, ulipatikana ukiwa umelala kitandani ukiwa uchi.

Muhtasari

•Mwili wa Naftali Nyadera ulipatikana Lavanda Lodging ambako alijivinjari na mpenzi wake usiku kucha.

•Mwanadada huyo anazuiliwa katika  kituo cha polisi  kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na kifo cha mpenzi huyo wake.

Image: MAKTABA

Polisi katika kaunti ya Migori wanamzuilia mwanadada mmoja wa miaka 24 baada ya mpenzi wake mwenye umri wa miaka 52 kupatikana amefariki ndani ya chumba cha kulala kukodisha.

Mwili wa Naftali Nyadera ulipatikana Ijumaa asubuhi katika chumba kimoja cha Lavanda Lodging iliyo West Kanyarwanda, eneo la Nyatike ambako alijivinjari na mpenzi wake usiku kucha.

Kitengo cha DCI kimeripoti kuwa mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa umelala kitandani huku ukiwa uchi.

Polisi kutoka kituo cha Macalder ambao walifika katika eneo la tukio baada ya kupokea taarifa walibaini kuwa marehemu alizirai masaa machache baada ya kuingia kwenye lodging hiyo akiandamana na mpenziwe.

"Mwili wa marehemu kwa sasa umehamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Migori Level 4, huku ukisubiri uchunguzi wa maiti kufanyika ili kubaini chanzo hasa cha kifo," Taarifa ya DCI imesema.

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa na wakati mzuri na mpenzi huyo mdogo kabla ya kupatikana amefariki.

Kwa sasa mwanadada huyo anazuiliwa katika  kituo cha polisi  kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na kifo cha mpenzi huyo wake.