Nyanya ya mtoto Junior Sagini ahusishwa katika kesi ya kumng'oa macho

Rael Nyakerario alifikishwa kizimbani pamoja na washukiwa wengine wawili

Muhtasari

•Upande wa mashtaka, hata hivyo, uliomba washukiwa wazuiliwe katika seli kwa siku moja zaidi ili kuruhusu wahusika wote kuhudhuria.

•Hivyo watarejeshwa mahakamani kesho kwa ajili ya kutajwa kwa kesi.

Pacifica Nyakerario alipofikishwa kortini Jumanne kwa jaribio la kumuua Mtoto Junior Sagini. Mshukiwa mmoja zaidi alikamatwa na atafikishwa mahakamani Alhamisi
Pacifica Nyakerario alipofikishwa kortini Jumanne kwa jaribio la kumuua Mtoto Junior Sagini. Mshukiwa mmoja zaidi alikamatwa na atafikishwa mahakamani Alhamisi
Image: MAGATI OBEBO

Mshukiwa wa tatu - nyanya- ameratibiwa kufikishwa katika mahakama ya Kisii kwa jaribio la kumuua mtoto Junior Sagini ambaye aling’olewa macho siku ya Alhamisi wiki iliyopita.

Rael Nyakerario alifikishwa kizimbani pamoja na washukiwa wengine wawili-Alex Ochogo na Pacifica Nyakerario mnamo Alhamisi.

Upande wa mashtaka, hata hivyo, uliomba washukiwa wazuiliwe katika seli kwa siku moja zaidi ili kuruhusu wahusika wote kuhudhuria.

“Ni kwa kuzingatia ukubwa wa kesi hii ndiyo maana tumezingatia maslahi ya pande nyingine zinazotaka kuwepo ndipo tunaiomba mahakama kutoa siku moja zaidi kwa washukiwa walioko rumande,” alisema Mwendesha Mashtaka Hillary Keino.

Hivyo watarejeshwa mahakamani kesho kwa ajili ya kutajwa kwa kesi.

Mtoto Sagini alitekwa nyara na wavamizi ambao wa walimng'oa macho, jambo ambalo limezua hasira kubwa kote nchini.

Serikali tayari imemhamisha mwathiriwa hadi katika nyumba salama jijini Nairobi.