Harmonize awasha stejini “Everybody say Wasafi!” Diamond Platnumz akosa (Video)

1522009524hh
1522009524hh
Staa wa Bongo Rajab Abdul almaarufu kama Harmonize na aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz walitarajiwa kukiwasha katika jukwaa moja fiesta kubwa London ila kutokana na kuchelewa kwa pasipoti. Dogo Harmonize alikuwa tayari ashafika jijini London kuwakonga nafsi mashabiki wake wa muziki.

https://www.instagram.com/p/B1injo8H13r/

Wengi walitarajia kuona ubishi wa maneno stejini. Stima za ushikaji kati ya mastaa hawa zilikata baada ya Harmonize kuwasilisha barua akitaka kuondoka katika lebo hiyo ya WCB. Akizungumza na runinga ya Wasafi, afisa mkuu mtendaji wa WCB Sallam alifichua kwamba katika nafsi yake hayupo katika lebo hiyo bali kimkataba. Aidha, Harmonize ameitisha mkutano na usimamizi wa WCB .

“Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi,” alisema Sallam.

“Siku ambayo atatoka kimkataba tutatangazia umma. Kwa sasa hivi ameandika barua. Nafsi yake imetoka WCB. Kufanya kazi ndani ya WCB, ndani ya moyo wake, haiko radhi tena,” aliongezea Sallam.