'Historia na utamaduni ndio ilinivutia Everton,' Carlo Ancelotti afunguka

ancelotti
ancelotti
Kocha mpya wa Everton,  Carlo Ancelotti amesema kilichomvutia kujiunga na klabu ya Everton ni: "Historia na utamaduni wa klabu hiyo kuwa kubwa zaidi England." Ancelotti ameshinda ligi ya mabingwa mara tatu kama kocha - mara mbili akiwa na AC Milan na mara moja na Real Madrid.

Ancelotti anasema kuigeuza klabu hiyo kuwa ya kugombea nafasi ya kucheza Champions League si jambo ambalo halitawezekana. Ancelotti, 60, anaichukua timu hiyo ikiwa katika nafasi ya 15 kwenye jedwali la Ligi ya Primia, wakiwa na alama nne tu juu ya mstari wa kushuka daraja.

Kocha huyo ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na AC Milan ametia saini mkataba wa kuwanoa Everton mpaka mwaka 2024.

Mkusanyiko wa habari za spoti;

Tottenham Hotspur wamefanya mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa Flamengo Gerson na ina mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa Brazili wa miaka 22 kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji mwezi Januari.

Mlinzi wa West Brom Mmisri Ahmed Hegazi, mwenye umri wa miaka 28, hakuchukuliwa na meneja Slaven Bilic kutokana na tukio lililotokea katika uwanja wa mazoezi.

United hawatamtoa kiungo wao wa kati Mserbia Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, ambaye mkataba wake mpya unamalizika mwezi Juni 2020.

Real Madrid wamemwambia ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola kwamba hawatomsaini kiungo huyo wa kati mwezi Januari.

Chelsea wamepewa fursa ya kumsaini Isco mwenye umri wa miaka 27 kwa dau la uro milioni 44 na Real Madrid, hatua itakayotoa fursa kwa mabingwa hao wa Uhispania kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham Christian.