Jinsi ya kuyatamka sawa majina ya wanamichezo nyota wa Afrika

nyota
nyota

Katika msururu wa barua za kutoka kwa waandishi wa Afrika, mwandishi wa Sierra Leone Ade Daramy anafafanuwa kwanini anakerwa anapoona Waafrika wanafanikiwa katika michezo.

Nilipotazama mashindano ya ubingwa wa riadha duniani huko Qatar, kama Muafrika mwingine, ilikuwa ni mshtuko kila aliposhinda mwanamichezo kutoka bara la Afrika.

Sio kwamba ni kuchukizwa na matokeo yao bali kilichonikera namna majina yao yalivyotamkwa na kukosewa yanapotajwa na watangazaji wa michezo.

Chukua mfano wa mwanaidha mshindi wa medali kadhaa Nafissatou Thiam kutoka Ubelgiji. Jina lake la pili bado linatamkwa kama "tee-am".

Kidokezo kikuu

Watangazaji soka hawana shida kulitamka jina la pili la mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta lakini wakashindwa kulitamka jina la pili lenye silabi mbili la Mohamed Diamé, aliyekuwa mchezaji wa timu yatifa ya Senegal anayeichezea Qatar hivi sasa.

Basi huu hapa muongozo kwa watangazaji michezo:

  • Diamé - halitamkwi "dee-ah-may", badala yake "Jammeh" kama jina la aliyekuwa rais wa Gambia Yahyah Jammeh
  • Jina la kwanza la nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal - Sadio Mané' halitamkwi "sah-dee-oh", badala yake "sah-jaw"
  • Jina la kwanza la mchezaji wa England Dele Alli limefupishwa kutoka jina la KiNigeria "Bamidele"
  • Jina la pili la mchezaji wa Stoke City Mame Biram Diouf, kutoka Senegal, halitamkwi "dee-oof", badaa yake "joof"
  • Badou Ndiaye pia ni mchezaji wa Stoke na jina lake la pili hutamkwa "nj-eye"
  • Aboubakar Kamara wa Fulham ambaye ana asili ya Mauritania - jina lake hutamkwa kama lilivyo "ka-ma-ra"
  • Jina la mwisho la Moussa Wagué wa Senegal, anayeichezea Barcelona, hutamkwa "wah-geh"

' Funika masikio'

Na haitoshi kwa mchezaji kama Pape Bouba Diop kufunga goli lililochangia kushindwa mabingwa watetezi Ufaransa katika mechi ya kwanza ya kombe la dunia mnamo 2202 au kwamba amecheza soka England kwa miaka minane, jina lake bado linakoseka.

Aliitwa "Papa Bouba Dee-op" - kwanza jina lake la awali linatamkwa "pap", na la pili linapotamkwa husikika kama "robe" neno la kizungu.

Ni jambo la kuiskitisha kwamba tunaliangazia hili leo miaka 17 baada ya kumalizika muda wake katika mchezo wa kulipwa kwasababu ingelikuwa vizuri kuiskia jina lake likitamkwa sawasawa angalau mara moja katika muda aliocheza.

Ushauri kwa waafrika ni kuhakikisha kwamba wana vitu viwili muhimu kila wanapofuatilia mashindano makubwa ya michezo: Televisheni kubwa na viziba masikio.

Kwahivyo iwapo watangazaji hawatoshughulika au hawatobadili namna wanavyoyatamka majina haya, itabidi tuvumilie tu katika mashindano yajayo ya kombe la dunia Qatar 2022.

-BBC