RIP Joe Kadenge:Rais Kenyatta aomboleza kifo cha Gwiji wa soka Kenya

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi  kwa familia  na rafiki za Joe akadenge  ambaye ameaga dunia siku ya jumapili katika  hospitali moja Nairobi akiwa na umri wa miaka 84 . rais Amesema marehemu Kadenge altumia  talanta yake kikamilifu kuihudumia nchi na kenya itamkosa mtu  muhimu sana aliyeipa kenya fahari kuu katika ulingo cha soka na michezo kwa jumla .

"Joe Kadenge  alikuwa kielelezo muhimu sana cha ubora wa  kandanda ya Kenya .Ni  huzuni kwamba mkono wa kifo umetupokonya  mtu aliyejitolea kuiletea Kenya fahari na taadhima wakati wake’ Rais amesema .Kadenge,  amekuwa akiugua kwa muda mrefu  na ametajwa kama mshambulaiji bora wa sokamabaye Kenya imewahi kuwa naye . msemo maarufu wa    'Kadenge na mpira'  ulitokana na umahiri wake alipokuwa akisakata  soka ,na watangazaji wengi wa mpira walikuwa wakisisimka sana wakati marehemu Kadenge alipokuwa na mpira uwanjani .

Miaka miwili iliyopita , Rais Kenyatta na Mama wa taifa   Margaret Kenyatta walimtembelea Kadenge aliyekuwa nyumbani kwake mtaani Mariakani jijini Nairobi   ili kumtakia nafuu  .‘Joe  alikuwa rafiki wangu ,alikuwa na maneno ya  busara alioniambia  wakati mimi na mama wa taifa Margaret tulipomtemebelea’ amekumbuka Rais .Joe Kadenge  alikuwa mwanasoka mahiri sana siku zake na aliichezea timu ya taifa Harambee stars  kwa miaka 14  baada ya kuanza kusakata boli  miaka   ya sitini . Baada ya kustaafu kutoka soka ,Joe alijitosa katika  usimamizi wa kandanda ambapo pia alipaa na kuwa kocha wa timu ya Haramve Stars mwaka wa 2002. Mwenyezi mungu na aijalie  nafsi yake na kuipa ujasiri familia na rafiki zake .