Ken Okoth - Vuta ni kuvute yazuka kuhusu kuuchoma au kuuzika mwili wake

OKOTH
OKOTH
Mvutano umeibuka kuhusu vile marehemu mbunge wa Kibra Ken Okoth atazikwa huku upande mmoja wa familia ukitaka mwili wake kuchoma na mwingine ukipinga hilo na kutaka azikwe.

Gazeti la The Star limebaini kwamba mamake Okoth ambaye anaugua, Angelina, ameonya dhidi ya mpango wa kuuchoma mwili wa mwanawe akisema kwamba atasusia mazishi ya mwanawe ikiwa msimamo wake hautazingatiwa. Okoth alifariki siku ya Ijumaa wiki iliyopita akipokea matibabu katika Nairobi Hospital baada ya kuugua ugonjwa wa saratani ya utumbo kwa muda.

Jamaa wa familia yake siku ya Jumanne alisema kwamba kuna hofu huenda afya ya Angelina ikazoroteka zaidi ikiwa ombi lake kumzika mwanawe nyumbani kwake Kasewe, Kaunti ya Homa bay litapuuzwa.

Malumbano pia ni baina ya jamaa wa upande wa babake na upande wa mamake kila upande ukitaka kuzika mwili wa Okoth.

Duru katika familia ziliarifu The Star kuwa mkewe Okoth, Monica ambaye ni wa asili ya bara uropa na kake mdogo wa Okoth wanashinikiza mwili wake kuchomwa, kulingana na ombi lake.  Mvutano huo unaohusisha Monica kuhusu mwili wa mumuwe unaleta kumbukumbu kuhusu vuta ni kivute ya mwaka 1986 iliyozingira mwili wa aliyekuwa wakili mahiri SM Otieno.

Hatimaye Otoiieno alizikwa myumbani kwao Siaya baada ya kipindi kirefu cha malumbano baina ya ukoo wa Umira Kager na mkewe Wambui Otieno.  Siku za hivi majuzi miili ya watu kadhaa mashuhuri wakiwemo wafanyibiashara, wanasiasa, viongozi wa makanisa na wanaspoti ilichomwa, licha ya wakati mwingine pingamizi kutoka kwa baadhi ya watu wa familia zao.

Wale ambao miili yao lichomwa kuambatana na maombi yao ni aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Bob Collymore, aliyekuwa kinara wa upinzani Kenneth Matiba, Aliyekuwa askafu mkuu wa kanisa la kiangilikana nchini Manasses Kuria na mkewe Mary, aliyekuwa waziri Peter Okondo, aliyekuwa msimamizi wa spoti Joshua Okuthe na mshindi wa tuzo ya Nobel Wangari Maathai.

Duru katika familia ya Marehemu Okoth zilisema kwamba mamake ameapa kutoambatana na mwili wa mwanawe ikiwa utarejeshwa tena Nairobi kuchomwa baada ya misa ya wafu katika eneo la Kasewe.