Kikosi changu kichanga kinaimarika kila siku - Solskjaer

Solskjaer
Solskjaer
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba kikosi chake chenye wachezaji wa umri mdogo kinaimarika kila uchao ikilinganishwa na vile walivyoanza msimu.

United imeshinda mara moja katika mechi zake sita za ligi ya Uingereza na ilihitaji penalti kuishinda klabu ya daraja la kwanza ya Rochdale katika michuano ya Carabao siku ya Jumatano.

''Sijasema kwamba itakuwa rahisi msimu huu'' , alisema mkufunzi huyo wa Man United.

''Kutakuwa na changamoto. Tunaposhindwa mechi lazima tujiamini na kile tunachofanya''.

Kikosi hicho cha Solkjaer ambacho kilishindwa 2-0 na West Ham wikendi iliopita , kitachuana na Arsenal katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumatatu usiku.

''Utamaduni upo, hatuna tatizo na jinsi wachezaji wanachukulia kila mechi, na viwango'' , aliongezea.

''Unaweza kuona dhidi ya Astana na Rochdale, wanataka kucheza vizuri na mara nyengine wanaharakisha mashambulizi yao''.

Siku ya Jumanne, klabu hiyo ilitangaza mapato yaliovunja rekodi ya £627m.

Ifuatayo ni msururu wa habari za spoti bara Uropa.

Mkataba wa ununuzi huo unadai kuwa meneja wa Newcastle manager Steve Bruce amepata mafanikio "yasiyoweza kulinganishwa Ulaya.

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, mwenye umri wa miaka 27, amewasili nchini Uhispania kwa ajili ya kesi dhidi ya klabu yake ya zamani Barcelona juu ya kusaini mkataba usio na malipo kuhusu faida.

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, atachukua hatua mpya ya kuondoka mwezi Januari.

Mkuu wa zamani wa Chelsea na Manchester United Peter Kenyon ameanza mchakato mpya wa kuinunua Newcastle kwa ushirikiano na mkewe kwa kumlipa mmiliki wake Mike Ashley pauni milioni 125 kwanza.

-BBC