Kocha wa Gor Mahia aruhusiwa kwenda nyumbani kushughulikia maswala ya kibinafsi

Gor Mahia jana ilithibitisha kwamba kocha mkuu Hassan Oktay amepewa siku kadha za mapumziko kushughulikia masuala ya kifamilia nyumbani kwao Uturuki.

Kocha huyo ataondoka kuelekea Uturuki hii leo na mabingwa hao wa KPL hawakusema anatarajiwa kuregea lini. Kocha huyo ameahidi kurudi kwani sio mara ya kwanza kwa kocha wa Gor Mahia kuondoka nchini kushughulikia masuala ya kibinafsi na kukosa kuregea.

Mwaka uliopita Dylan Kerr aliondoka nchini kwa sababu kama hizo na akaishia kujiuzulu.

Kiungo wa Gor Mahia Dennis Oliech ameregelea mazoezi na klabu hio baada ya kupona jeraha. Oliech aliyesajiliwa Gor Mahia mapema mwaka huu alikatazwa kukamilisha msimu Mei baada ya kuvunjika mkono na alidhaniwa kuwa huenda angekaa nje kwa miezi mitano.

Hata hivyo anaripotiwa kupona na kuanza mazoezi na timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Kogallo itamtegemea sana Oliech msimu huu baada ya kuondoka kwa Jacques Tuyisenge ambaye amehamia Angola.

Kwingineko, Nicolas Pepe anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Arsenal katika kipindi cha siku chache zijazo baada ya mkataba kuafikiwa na Lille.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 24 anatarajiwa kuwa mchezaji wa Arsenal wiki hii na atakua wanne kusajiliwa na msimu huu wa joto. Pepe alifunga mabao 22 katika Ligue 1 msimu uliopita, na kuibuka wa pili nyuma ya Kylian Mbappe wa Paris- Saint Germain, na kusaidia mara 11, Lille ilipomaliza nyuma ya PSG.

Gareth Bale hajajumuishwa katika kikosi cha Real Madrid kitakachosafiri kuelekea Ujerumani kabla ya msimu kuanza. Miamba hao wa Uhispania wamesema katika tovuti yao kuwa Bale hajafanya mazoezi nje ya kikosi hicho, badala yake amefanya mazoezi ndani na mchezaji mwenzake aliye na jeraha Luka Jovic.

Real ilitangaza kwamba kikosi hicho kinachoelekea Munich na jina la Bale halikuwa kwenye orodha hiyo ya wachezaji 24. Inaarifiwa kwamba Bale hayuko tayari kucheza baada ya rais wa Real Florentino Perez kumzuia kujiunga na Jiangsu Suning.

Everton imewasilisha ombi la pauni milioni 55 pesa taslimu kumsajili kiungo wa Crystal Palace Wilfried Zaha huku kukiwa hakuna mchezaji wanayejitolea kubadilishana na wapinzani wao katika ligi ya Premier.

Palace inataka pauni milioni 60m awali ili kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast na pia ina wasiwasi kuhusu namna Everton inavyotaka kupangia malipo katika makubaliano yoyote yanayowezekana kuidhinishwa.

Inter Milan bado wanafanya majadiliano ya kumsajili mshambulizi wa Manchester United Romelu Lukaku kwa mujibu wa mkurugenzi wa Inter Beppe Marotta.

Lukaku amewachwa nje ya kikosi cha United kilichosafiri kwa mechi ya leo ya kirafiki dhid ya Kristiansund huko Norway, na amekosa mechi zote nne za kabla ya msimu kuanza huko Australia, Singapore na Uchina kutokana na jeraha dogo.

Juventus wanatayarisha ofa ya kumtaka Lukaku na wako tayari kumjumuisha Paulo Dybala kama sehemu ya makubaliano yao, lakini raia huyo wa Argentina anataka kusalia Turin.