Lampard asema yupo tayari kukabiliana na mtihani wa pili hii leo

Baada ya kucharazwa magoli manne bila jibu na klabu ya Manchester United ugani Old Trafford, Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema kuwa yuko tayari kuonyesha ulimwengu uwezo wake kwenye mechi ya fainali ya super cup hii leo dhidi ya Liverpool.

UEFA super cup hushindaniwa na mshindi wa klabu bingwa barani Ulaya pamoja na mshindi wa ligi ya Europa.

Klabu ya Bayern Munich imekamilisha uhamisho wa mshambulizi wa Inter Milan na Croatia,Ivan Perisic kwa mkopo kwa ada ya pauni millioni nne. Perisic ambaye amejipaa katika hali tatanishi hivi karibuni kufuatia ujio wake Antonio Conte. Perisic ana umri wa miaka 30.

Mshambulizi wa Ufaransa, Wissam Ben Yedder amekamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Monaco akitokea Sevilla ya Uhispania.Monaco ililazimika kutoa kitita cha pauni millioni thelathini na tano. Kwenye ada hio, Mshambulizi antony Lopes ameelekea Sevila pia.