Manchester United inapania kumlipa Pogba, pauni nusu milioni kila wiki

Manchester United inapania kumlipa Paul Pogba, 26, hadi pauni nusu milioni kwa wiki licha ya Real Madrid na Juventus kumnyatia kiungo huyo raia wa Ufaransa.

Hata hivyo, Crystal Palace imekataa ombi la Manchester United la puani millioni  50m la kutaka kumsajili beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka. United mwanzo walitoa pauni millioni 35m, na pia kukubali kuongeza pauni millioni 15m baadae.

Tukisalia uingereza, kocha wa Derby Frank Lampard anajiandaa kukutana na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kujadiliana kuhusu uwezekano wake kuchukua nafasi ilioachwa wazi na Maurizio Sarri, ambaye alijiunga na Juventus wiki iliyopita.

Kwingineko, klabu ya Bayern Munich inataka kumsajli kwa mkopo winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale, 29.

Kiungo wa klabu ya Lyon Mfaransa Tanguy Ndombele, 22, amesema kuwa anaweza kuhamia Tottenham kama nafasi itatokea.

Mbali na kadanda, mchezaji nambari moja wa tenisi wa hapo awali Andy Murray anasema oparesheni yake ya kiuno imebadilisha maisha yake, na anatarajia kurejea katika mchezo huo.

Murray atacheza katika mchezo wa doubles na mwenzake Feliciano Lopez wiki ijayo. Anarejea ulingoni miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji na huenda akarejea kikamilifu baadae mwaka huu.