Manchester United yamsajili beki ghali zaidi Ulimwenguni

EBNBQ-2XkAAdij1
EBNBQ-2XkAAdij1
Klabu ya Manchester United imevunja rekodi ya ada iliyolipwa kumnunua beki yeyote ulimweguni baada ya kumsajili Harry Maguire kutoka Leicester City kwa ada ya millioni 85.

Maguire ametia sahihi mkataba wa miaka sita na Manchester United.

 Maguire mwenye umri wa miaka 26 amekuwa beki ghali zaidi ulimwenguni akimpita Virgil Van Dirk aliyejiunga na Liverpool mwaka jana mwezi januari kwa kitita cha millioni 75 akitokea Southampton ya Uingereza. Maguire anakuwa mchezaji wa pili mwenye bei ghali zaidi Ugani Old Trafford  baada ya Paul Pogba.
"Asanteni kwa watu wote waliochangia kwa maisha yangu ya soka hadi Kufikia sasa. Nina furaha kuwa mchezaji ugani Old Trafford kwani ni ndoto ya kila mtoto kuchezea Manchester United."

Maguire alianzia maisha yake ya soka katika klabu ya Sheffield United kabla ya kujiunga na klabu ya Hull City. Mnamo mwaka wa 2016,Maguire aliisaidia Hull city kupandishwa daraja na kujiunga na ligi Kuu nchini Uingereza.

Mwaka 2017, Maguire alikamilisha uhamisho wake kwenda Leicester City kwa ada ya millioni 17huku akicheza mechi 69 ndani ya muda wa miaka miwili.
Aidha, alichezea taifa lake mechi yake ya kwanza mwaka wa 2017 mwezi Agosti huku akiisaidia kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mechi za kombe la dunia mwaka uliopita kule nchini Urusi.