Mastaa watano wakiafrika walioshindwa kulitwaa kombe la Afcon

Dimba la AFCON linafikia kikomo hii leo kule nchini misri huku taifa la Algeria likimenyana na Senegal kwenye mchuano wa Fainali.

Hatahivyo, katika historia ya Afcon, kunao mastaa walliotesa barani ulaya ila wakashindwa kufanyia mataifa yao vivyo hivyo.

Wenye mchuano huo macho yote ya mashabiki wa Senegal yataelekezwa kwake Sadio Mane aliyeisaidia Liverpool kutwa kombe la klabu bingwa barani ulaya msimu uliopita.

Riyad Mahrez kwa upande mwingine anatarajiwa kuwaongoza Algeria kutafta taji lake la kwanza kwa taifa lake.

Didier Drogba

Drogba ameliwakilisha taifa la Ivory Coast kwenye michuano sita ya Afcon.

Kwenye awamu hizo zote alizoiwakilisha Ivory Cokast, Drogba alifika fainali mara mbili huku akipoteza fainali hizo zote kupitia njia ya Penalti. Drogba anakumbukwa sana na mashabiki wa Chelsea kwa goli alilowafunga Bayern Munich mwaka 2012. Katika maisha yake hajawahi shinda taji la Afcon.

George Weah

George Weah ndiye mchezaji bora kuwahi kutokea bara la Afrika. Alikuwa mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la mchezaji bora wa mwaka duniani kote 'Ballon D' Or'. Weah akiliwakilisha taifa la Liberia hajawahi kulishika taji la Afcon licha ya kukitesa barani ulaya kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Michael Essien

Essien alikuwa kiungo mkabaji kutokea taifa la Ghana. Hata hivyo, mkali huyu aliyechezea timu ya Chelsea na Real Madrid alishindwa kuleta taji la AFCON nchini Ghana.

MIchael Essien alikubwa namajeraha ya mara kwa mara jambo lililomkosesha mechi nyingine za AFCON. Atayakumbuka majeraha yake kwa kumkosesha mechi ya robo fainali dhidi ya Uruguay.

Kkatika historia ya Afcon,kunao mastaa walliotesa barani ulaya ila wakashindwa kufanyia mataifa yao vivyo hivyo.Kkatika historia ya Afcon,kunao mastaa walliotesa barani ulaya ila wakashindwa kufanyia mataifa yao vivyo hivyo.

Seidou Keita

Keita ni mmoja wa viungo bora kuwahi kusakata soka kutoka bara la Africa.

Keita aliwakilisha taifa la Mali kwenye michuano ya Afcon Mara saba huku akishindwa kutwaa taji hilo hata mara moja.

Keita ameshinda taji la klabu bingwa barani ulaya mara mbili na Barcelona ila akirejea nyumbani kwao Mali kitoweo chake kilingia mchanga.

Nwankwo Kanu

Licha ya kutwa taji la UEFA pamoja na ligi kuu nchini uingereza, Kanu hakushinda taji la Afcon akiliwakilisha taifa la Nigeria kuanzia mwaka wa 1995 hadi 2010.

Kanu alistaafu soka la kimataifa baada ya Nigeria kubandul;iwa kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 kule nchini Afrika kusini.

Hata hivyo, Kanu aliliwakilisha taifa la Nigeria kwenye michuano mitatu ya kombe la dunia.