https://radiojambo.co.ke/picha-ya-siku-maelfu-ya-watanzania-wajitokeza-kutizama-mbwana-samatta/
Shirikisho la soka nchini FKF jana lilizindua bodi itakayosimamia uchaguzi utakaofanyika Machi tarehe 30. Bodi hilo itaongozwa na Kentice Tikolo, Patrick Onyango, Ali Hassan, Alfred Ndinya, na Samuel Karanja. Watasmamia kura hizo za kitaifa na zile za kaunti na pia kuwachagua watakaoongoza kura za mashinani. Uchaguzi hio ulismamishwa mwezi Disemba mwaka 2019 baada ya wagombeaji kukosa imani na bodi iilyotajwa.
Wajumbe 25 kutoka shirikisho la riadha duniani IAAF, wanatarajiwa nchini wiki ijayo ili kufanya uchunguzi kabla ya Kenya kuandaa mbio za ubingwa duniani za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20. Wajumbe hao watakagua uwanja wa Kasarni, chuo kikuu cha Kenyatta ambako wanariadha wanatarajiwa kupiga kambi, na hoteli jijini Nairobi. Rais wa shikrikisho la ridha nchini Jackson Tuwei, anasema wajumbe hao wataongozwa na mkuu wa mawasiliano wa IAAF Jacky Brock.
Ajenti wa Gareth Bale Jonathan Barnett anasema hadhanii kama mteja wake atawahi kuregea Tottenham tena. Raia huyo wa Wales aliondoka Spurs na kuelekea Real Madrid mwaka wa 2013 kwa kitita cha pauni milioni 85 wakati huo. Kumekua na tetesi katika siku za hivi majuzi zilizomuhusisha Bale na kuregea Tottenham mwezi uliopita huku ripoti zikiashiria kwamba vilabu hivyo vilikua katika majadiliano. Barnett anasisitiza kwamba klabu hio ya North London haijawasilisha ofa yoyote kwa ajili ya Bale. Hatma ya Bale imekua ikijadiliwa sana tangu Zinedine Zidane aregee kwenye klabu hio.
Real Madrid wanapanga kuwasilisha ofa ya pauni milioni 250 kumnasa kiungo wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe. Mchezaji huyo wa miaka 21 raia wa Ufaransa alilumbana na meneja wa PSG Thomas Tuchel baada ya kuondolewa uwanjani wakati walipowafunga Montpellier mabao 5-0 siku ya Jumamosi. Uhusiano wa waili hao unasemekana kudorora na Mbappe huenda akaondoka.