Michezo 2

Mechi za kombe la mabingwa,awamu ya 16 bora

Tottenham Vs RB Leipzig

Tottenham  italazimika kujitolea kwa njia zote ili kubatilisha   kushindwa kwao katika awamu ya kwanza ya mechi za kombe la mabingwa za 16 bora leo watakapochuana na  RB Leipzig,  amesema  maneja  Jose Mourinho.Leipzig  walishinda mchuano huo wa mkondo wa kwanza bao moja kwa nunge kwa hisani ya  mkwaju wa penati wa Timo Werner.Spurs  walifuzu kwa fainali ya kombe hilo msimu uliopita chini ya kocha wao wa zamani  Mauricio Pochettino

Valencia vs Atalanta

Valencia  italenga kujaribu kubatilisha kushindwa  mabao manne kwa moja dhidi ya Atalanta  katika mchuano wa mkondo wa pili wa kombe la mabingwa  katika uwanja wa  Mestalla  kwenye mechi itakayochezwa kbila mashabiki kwa ajili ya hofu ya virusi vya Corona . wenyeji watakosa huduma za mshambuliaji  Maxi Gomez (jeraha la kuvunjika mguu)  na mlinzi  Ezequiel Garay (goti ) . Mlinzi  Gabriel Paulista  pia atakuwa nje ya kikosi hicho .Atalanta kwa upande wao  wanatilia shaka uwezekano wa kuwepo kwa difenda wa Brazil  Rafael Toloi

 

 

Photo Credits: Yusuf Juma

Read More:

Comments

comments