Michezo, Odsonne Eduoardo hatoshi mboga -Asema Charlie Nicholas

54512191_2314673208804928_2948301863352707755_n
54512191_2314673208804928_2948301863352707755_n
NA NICKSON TOSI

Itamchukuwa muda mwingi kwa mshambulizi wa Celtic  Odsonne Edouard kutulia katika ligi kuu ya Uingereza na hata kuwa vigumu kuridhi mikopa itakayoachwa na mshambulizi wa sasa wa klabu ya Arsenal Pierre -Emerick Aubameyang. Haya ni kulingana na mchanganuzi wa michezo Charlie Nicholas.

Eduorado amepigiwa upato kuchukuwa nafasi itakayoachwa na mshambulizi wa Arsenal Aubameyang baada ya mkataba wake kukamilika Juni mwaka huu, huku klabu ya Bercelona ikiwazia kumsajili mcheza huyo wa Gabon. Eduardo amefunga magoli 28  katika mechi 62 ambazo amezichezea klabu ya Celtic msimu huu.

Ligi kuu ya Scotland ilisitishwa kutokana na mkurupuko wa Virusi bvya Corona ambapo mataifa takriban 196 kote ulimewenguni yanaripotiwa kuathirika na virusi hivyo.

Mashabiki wa klabu ya Celtic wamekuwa wakimlinganisha Eduardo na mshambulizi wao wa zamani Ousaman Dembele kutokana na mchezo wake mahiri na namna anavyotinga magoli .

Dembele aliuzwa na Celtic katika klabu inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Lyon kwa kima cha Euro milioni 19.7 mwaka 2018.