Pep Guardiola asema kuwa angetaka Leroy Sane kusalia ugani Etihad

leroy sane
leroy sane
Pep Guardiola anasema anamtaka Leroy Sane kusalia Manchester City lakini anakiri kuwa uamuzi huo si wake. Sane ana miaka miwili iliyosalia kwenye mkataba wake lakini hajasema lolote kuhusu majadiliano ya kuuongeza mkataba.

Bayern Munich inataka kumsajili Sane. Bayern ilifanya majadiliano na wawakilishi wa Sane mapema wiki hii kuhusiana na uwezekano wa uhamisho Allianz Arena.

City hawataki kumuuza Sane na bado hawajapokea ofa rasmi kwa ajili ya wing'a huyo Mjerumani.

Everton wanataka kumsajili Wilfried Zaha na watafanya majadiliano kuhusu uhamisho wake wiki hii. Zaha angetaka kuhamia Arsenal, lakini Crystal Palace wanadinda kumuuza Zaha kwa the Gunners mpaka thamani yao ya pauni milioni 80 itimizwe.

Arsenal hawajakata tamaa ya kumsajili mchezaji huyo wa umri wa miaka 26 na wanatarajiwa kuwasilisha ofa nyingine wiki hii lakini sasa watakabiliwa na ushindani kutoka Everton.

The Eagles hawana haraka ya kumuuza Zaha kwani wameshamuuza Aaron Wan Bissak kwa Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 50.

Bruno Fernandes anayelengwa na Man United alifunga bao moja na kusaidia lingine Liverpool walipomaliza ziara yao ya Marekani kwa sare ya 2-2 na Sporting Lisbon.

Kiungo huyo wa kati mreno alifunga baada ya dakika tano ugani Yankee Stadium. Liverpool wakajibu kupitia kwa Divock Origi na Giorginio Wijnaldum kabla ya muda wa mapumziko.

Sporting wakasawazisha dakika 9 katika kipindi cha pili kupitia kwa Fernandes. Liverpool watachuana na Napoli watakaporejea Uingereza.

Kocha mpya wa All African Games Musa Benjamin anasema atasisitiza masuala msingi katika jitihada za kupiga jeki nafasi ya Kenya kupata medali huko Morocco.

Kocha huyo wa AIBA anasema wanandondi wengi katika kikosi hicho cha watu 26 wanahitaji usaidizi kabla ya kuingia katika ngazi ngumu ya mchezo huo. Musa anasema kwamba wanandondi wote watakusanyika katika kambi hapo kesho.