Mshambuliaji wa wales Gareth Bale hajawahi kuzungumza kuhusu kuondoka Real Madrid, amesema kocha Zinedine Zidane. Bale, mwenye umri wa miaka 30, alitarajiwa kujiunga na kilabu ya uchina Jiangsu Suning lakini uhamisho huo ukafeli.
Bulgaria imeagizwa kucheza mechi mbili bila mashabiki uwanjani huku mchuano mmoja ukitarajiwa kuchezwa baada ya miaka miwili kwa hatua ya mashabiki wake kuwatukana wachezaji weusi wa England wakati wa mchuano wa kufuzu kwa kombe la Euro mwaka ujao.
England ilishinda Bulagria mabao sita kwa nunge huko sofia katika mechi ambayo nusra isitishwe iwapo wachezaji wa England hawangeamua kuimaliza.
Tukirejea nchini, mchezaji wa kikosi cha raga cha Sevens Collins Injera atakosa mchuano wa kufuzu kwa mechi za olimpiki mwaka ujao mjini Tokyo uliopangwa kusakatwa kati ya novemba tarehe 8 hadi 9 nchini afrika kusini.
Hata hivyo maneja wa timu Eric Ogweno amethibitisha kwamba Injera aliyejeruhiwa bega wakati wa mechi za safari sevens atakuwa katika hali nzuri kushiriki mechi za msururu wa IRB msimu wa 2019/2020 mwezi disemba.