Neymar alilazimisha uhamisho wake kutoka klabu ya Barcelona na kujiunga na miamba wa Ufaransa PSG ila kwa sasa kitubua kimeingia mchanga.
Barani Ulaya tumeshuhudia mastaa wakilazimisha uhamisho kutoka klabu moja hadi nyingine ila baada ya uhamisho wakabaki kuwa makopo tu.
Thibaut Courtois
Dimitri Payet
Baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Mersaille ya Ufaransa, Payet alijitabulisha kuwa kipenzi cha wengi ugani London Stadium huku akiwachangamsha mashabiki wa klabu ya Westham na kuwapa hamu ya ushindi kwa mara nyingine. Januari mwaka 2016, Payet na mkufunzi wa Westham, Slaven Bilic walikosana jambo lilopelekea Payet kuandika barua akitaka kuigura klabu hio. Kama ilivyo kwa Courtois, Payet aligoma wiki mbili jambo lilopelekea WestHam United kumuza tena klabuni Mersaille.
Phillipe Coutinho
Diego Costa
Diego Costa anatabulikana kwa kupenda vurugu uwanjani licha ya kuwa yeye ni chui mbele ya lango. Baada ya kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza, aliyekuwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte alimwambia Fiego hamuhitaji jambo lilopeleka Costa kugoma kurejea Uingereza akidai auzwe au sivyo hatocheza tena. Baada ya vuta nikuvute nyingi, Costa aliishia kujiunga na Atletico Madrid na msimu uliopita alicheka na wavu mara tatu pekee.
Laurent Koscienly
Koscienly ameigura klabu ya Arsenal baada ya miaka tisda ugani Emirates. Mlinzi huyu mwenye umri wa miaka 33 alikuwa beki tegemezi kwa zaidi ya miaka minane hadi akawa nahodha wa kikosi hicho. Hata hivyo, mwezi juni mwaka huu, Koscienly aligoma kusafiri na Arsenal na kulazimisha uhamisho kwenda klabu ya Bordeaux ya Ufaransa. Kilichotia chumvi zaidi ni jinsi alivyojiwasilisha klabuni hapo baada ya kuvalia jezi ya Arsenal na kisha kuivua na kubaki na jezi yake mpya.