Mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia ya marathon awali alikuwa ametuzwa kama mwanaspoti bora baada ya kumpiku bingwa wa mbio za mita 1500 Timothy Cheruiyot na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za dunia za half marathon Geoffrey Kamworor.
" Uhuru upo katika michezo’ amesema Kipchoge .
Gwiji wa soka wa Nigeria Victor Ikpeba ndiye aliyekuwa mgeni staa katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na waziri wa spoti Amina Mohammed ,katibu wa kudumu wa wizara hiyo Joe Okudo na rais wa NOK Paul Tergat ambaye pia ndiye mwanzilishi wa tuzo ya Soya . Bingwa wa dunia katika mbio za mita 5000 Hellen Obiri ndiye alieyeshinda tuzo ya mwanaspoti bora wa kike mwaka huu .mshililizi wa rekodi ya mbio za marathon Brigid Kosgei alimalia wa pili ilhali bingwa wa marathon dunia Ruth Chepng'etich alimaliza wa tatu .