Marufuku ya FIFA yanukia Kenya-Nick Mwendwa asema hakuna pesa za kulimpa Adel

NA NICKSON TOSI

Rais wa shirikisho la Soka nchini Nick Mwendwa amesema hawako katika mpango wowote wa kumlipa mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa Adel Amrouche kima cha milioni 109 kama ilivyopendekezwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Agizo la FIFA la kutaka Kenya iwe imemlipa mkufunzi huyo senti zake inakamilika wiki hili.

Baada ya mkufunzi huyo kufutwa na usimamizi wa soka la humu nchini, aliishtaki Kenya katika mahakama ya kutatua migogoro ya michezo na kuamuliwa kuwa alipwe pesa hizo kabla ya Aprili 24 mwezi huu ambapo ni wiki hii.

Je Kenya itakwepa adhabu ya FIFA