Bayern Munich wako tayari kulipa £60m ili kumpata Leroy Sane

_112040543_461bbcb7-cef4-4f0d-a427-9acf31582962
_112040543_461bbcb7-cef4-4f0d-a427-9acf31582962

Bayern Munich wako tayari kulipa £60m tu kumnunua winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24. (Sky Sports)


Arsenal wameripotiwa kuwasiliana na Real Madrid kuhusu uhamisho wa beki wa Uhispania Sergio Reguilon, 23, ambaye yupo Sevilla kwa mkopo. (ABC, via Star)

Barcelona haitamuuza winga wa Brazil Philippe Coutinho kwa bei ya chini ya euro milioni 100 sawa na (£87m). Chelsea wamehusishwa na kiungo huyo matata wa miaka 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester City wameanza kujadiliana na Barcelona kumhusu beki wa Portugal Nelson Semedo, 26. Mkataba huo utamjumuisha beki mwezake wa Portugal Joao Cancelo, 25, kujiunga na upande mwingine. (Sport)

Arsenal wameambiwa lazima walipe zaidi ya £25m ikiwa wanataka kumnunua mshambuliaji wa Celtic na Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Express)

Mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens, 32, anataka kuhamia London, huku Chelsea ikiwa bado inamnyatia kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. (Mail)