Mchezaji wa cameroon Joseph Bouasse aaga dunia

Ulimwengu wa soka bara Afrika waomboleza kufuatia kifo cha kushangaza cha mchezaji soka wa Cameroon mwenye miaka 21, Joseph Bouasse ambaye aliaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo.

Bouasse, ambaye alihamia Italia akitokea Cameroon akiwa na miaka 16, alikuwa mwingi wa matumaini ya kuimarisha taaluma yake alifariki Jumapili, Mei 24.

Mchezaji huyo aliwakilisha timu ya akademia ya AS Roma kufuatia kufuzu kwake mwaka 2016.

Hata hivyo, hakupata nafasi ya kuchezea timu ya kwanza, alikabithiwa nafasi ya kipekee kufanya mazoezi na Daniele De Rossi na Francesco Totti jijini Rome.

https://twitter.com/wejinyasam/status/1264916441511481349

Mchezaji wa ESPN Andrew Cesare ametambua kufuzu kwa Bouasse jijini Roma ilikujia baada ya kuwachwa katika stesheni ya treni na mlanguzi ambaye alikuwa amemuahidi kumpatia maisha bora ughaibuni.

Alianza taaluma yake katika klabu cha daraja ya chini Italia, Vicenza huku akiwa kwa mkopo akitokea Roma mwaka 2017. Kabla ya kifo chake, Bouasse alikuwa mchezaji wa timu ya Romania, Universitatea Cluj ambapo alijiunga nao  Februari.