Mshambulizi wa Arsenal Aubameyang alikuwa tayari kuhamia Chelsea Januari

LONDON, ENGLAND - AUGUST 01: Pierre-Emerick Aubameyang of Arsenal is fouled by Cesar Azpilicueta of Chelsea leading to Arsenal being awarded a penalty during the FA Cup Final match between Arsenal and Chelsea at Wembley Stadium on August 01, 2020 in London, England. Football Stadiums around Europe remain empty due to the Coronavirus Pandemic as Government social distancing laws prohibit fans inside venues resulting in all fixtures being played behind closed doors. (Photo by Marc Atkins/Getty Images)
LONDON, ENGLAND - AUGUST 01: Pierre-Emerick Aubameyang of Arsenal is fouled by Cesar Azpilicueta of Chelsea leading to Arsenal being awarded a penalty during the FA Cup Final match between Arsenal and Chelsea at Wembley Stadium on August 01, 2020 in London, England. Football Stadiums around Europe remain empty due to the Coronavirus Pandemic as Government social distancing laws prohibit fans inside venues resulting in all fixtures being played behind closed doors. (Photo by Marc Atkins/Getty Images)

Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang alikuwa tayari kuhamia Chelsea Januari lakini Blues ikashindwa kutimiza matakwa ya mchezaji huyo, 31. (Mailonline)

Chelsea inakaribia kukukubali maafikiano ya uhamisho na Bayer Leverkusen kwa mchezaji wa Ujerumani, 21, Kai Havertz. (Teamtalk)

Barcelona imemfanya mchezaji wa Manchester City, 19, raia wa Uhispania beki wa kati Eric Garcia mlengwa wao mkuu kipindi cha usajili kitakapofunguliwa msimu huu. (Goal.com)

Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema kwamba beki wa kati wa Senegal Kalidou Koulibaly anaweza kuruhusiwa kuhama klabu hiyo ikiwa kiwango cha thamani yake cha pauni milioni 81 kitafikiwa. (Sky Italia, via Metro)

Kocha Ole Gunnar Solskjaer anataka Manchester United kuongeza kasi ya kumsaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho, 20, kuepuka hatua ya mvutano iliyojitokeza msimu uliopita kwa Harry Maguire. (ESPN)

Borussia Dortmund inaweza kujaribu kumsajili winga wa Uholanzi na aliyekuwa Manchester United Memphis Depay, 26, kutoka Lyon ikiwa United itamsajili Sancho. (Bild - in German)

Everton imetoa pauni milioni 18m kwa beki wa kushoto raia wa Uhispania wa Real Madrid, 23, Sergio Reguilon. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 28, amepata ofa ya Arsenal na Tottenham Hotspur, huku kukiwa na uwezekano wa Gunners kumsajili raia huyo wa Brazil na Barca ikipata pauni milioni 9 na kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 21. (Independent)

Fulham, Bournemouth na Stoke City zote zinamnyapia mshambuliaji wa Uingereza, 21, Mallik Wilks, ambaye ndio amejiunga na Hull City kwa mkataba wa kudumu mwezi uliopita. (Football Insider)

Barcelona na Inter Miami inayoongozwa na David Beckham zimetoa ofa ya mkataba kwa winga wa Chelsea raia wa Brazil Willian, 31. (Sky Sports)

Real Betis imeonesha nia ya kumsajili mlengwa wa Arsenal Dani Ceballos. Kiungo huyo wa kati, 23, yuko kwa mkopo Arsenal kutoka Real Madrid. (Onda Cero, via Sun)

Mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, 28, amewaambia wachezaji wenzake anataka kuondoka ili ajiunge na Ligi ya Premier kuendeleza matumaini yake ya Uingereza. (Telegraph)

Manchester United itahitajika kufahamishwa ikiwa Borussia Dortmund itatoa kima cha kumsaka Depay kwasababu ya kipengee walichokiweka kwenye makubaliano wakati inamuuza raia huyo wa Uholanzi kwa Lyon. (Star).

-BBC