Ronaldo anataka Juventus imsajili Raul Jimenez kutoka Wolves

Roro
Roro

Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo anataka Juventus kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Mexico Raul Jimenez, 29, kutoka Wolves kuwa mlengwa wao mkuu msimu ujao. (Gazzetta dello Sport, via Express)

Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo, 31, hana nia ya kujiunga na Paris St-Germain licha ya taarifa kwamba klabu hiyo ya Ufaransa ina nia ya kumsajili raia huyo wa Nigeria, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua hadi Januari. (Manchester Evening News)

Lille imekataa ofa ya euro milioni 20 euro kutoka kwa Everton kwa ajili ya mlinzi Gabriel, 22, kwasababu wana makubaliano ya kumuuza mchezaji huyo kwa Napoli, licha ya Arsenal na Manchester United pia kuonesha nia ya kutaka kumsajili raia huyo wa Brazil. (Gianluca di Marzio)

Newcastle inanyatia kumsajili mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye msimu uliopita alikuwa Roma kwa mkopo na pia analengwa na iliyokuwa klabu yake Fulham. (Newcastle Chronicle)

Mlinda lango wa Arsenal Emiliano Martinez anasema vilabu 10 Ulaya vimeonesha nia ya kumsajili baada ya mchezaji huyo, 27, raia wa Argentine kuonesha mchezo wa kuridhisha kuelekea mwisho wa msimu. (Marca - in Spanish).

-BBC