Chelsea inapania kumnunua mshambulizi wao wa zamani, Romelu Lukaku

lukaku. Picha: BBC
lukaku. Picha: BBC

Chelsea inafikiria kwamba itamnunua mchezaji wa Ubeljigi na aliyekuwa mshambuliaji wa Blues Romelu Lukaku, 27, ikiwa itashindwa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, msimu huu.

Manchester City pia ina mnyatia Lukaku, ambaye amefunga mabao 59 baada kuchezea mechi 85 Inter Milan.

Romelu Lukaku alisaidia Ubelgiji kupata alama moja katika mechi yao ya kufuzu Kombe la Dunia na Jamhuri ya Czech huko Prague. Lukas Provod alitanguliza kuweka mbele wenyeji. kabla ya Lukaku kufunga bao la kusawazisha.

Mshambuliaji huyo wa Inter Milan amefunga mabao 36 katika mechi 31 zilizopita za kimataifa - . Czech wako juu ya Ubelgiji, ambao wameorodheshwa nambari moja ulimwenguni, kwa tofauti ya mabao baada ya michezo miwili.

Paris St-Germain ina matumaini kuwa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, atasaini mkataba wa miaka minne zaidi lakini hatma ya Kylian Mbappe haijulikani. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 22, unamalizika mwaka 2022.

Mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 28, amedokeza kwamba anataka kusalia Liverpool - hata ikiwa upande wa kocha Jurgen Klopp utashindwa kuingia katika Ligi ya Mambingwa msimu ujao.

Manchester United iko tayari kumpokea kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28 msimu huu ambaye sasa hivi yuko kwa mkopo West Ham - na huenda kukawa na mazungumzo ya kuongezwa kwa mkataba wake.