Edinson Cavani asisitiza nia ya kuondoka Manchester United

cavani
cavani

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34, amekutana maafisa wa Manchester United na kusisitiza azma yake ya kutaka kuondoka klabu hiyo kurejea Amerika Kusini kuwa karibu na familia yake. Katika miezi ya hivi karibuni Cavani amehusishwa pakubwa na uhamisho wa kwenda Boca Juniors. (Depo - in Spanish)

Zifuatazo ni tetesi za soka ulimwenguni;

Matumaini ya Manchester United kumsajil mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 21, kutoka Borussia Dortmund huenda yamepata nguvu mpya kutokana na taarifa kwamba naibu mwenyekiti Ed Woodward anatarajiwa kuondoka klabu hiyo. (Star)

West Ham wameungana na Barcelona, Bayern Munich na Tottenham katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Norwich City na England wa chini ya miaka -21 Max Aarons, huku klabu hiyo ya Ligi ya Premia ikisemekana kuitisha angalau paundi milioni 30. (Independent)

Burnley wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Algeria Nabil Bentaleb kutoka Schalke msimu huu wa joto, ijapokuwa mchezaji huyuo aliye na umri wa miaka 26- ambaye huenda huenda akasalia bila timu hatarajiwi kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Ujerumani. (Sun)

Meneja Dean Smith anasema Aston Villa haina mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea na England Ross Barkley, 27, kwa mkataba wa kudumu wakati mkopo wake utakapokamilika mwisho wa huu. (Mirror)

Juventus itakuwa tayari kumtoa kiungo wa kati Ufaransa Adrien Rabiot,26, kwa Manchester United kama sehemu mpango wa kumpata mlinzi wa Brazil Alex Telles, 28. (Calciomercato - in Italian)

Roma wanajiandaa kukutana na wawakilishi wa Jannik Vestergaard wanaposhughulikia mpango wa kumsajili mlinzi wa Southampton na Denmark, 28, ambaye pia anasakwa na Tottenham na Juventus.(Tuttomercatoweb - in Italian)

Winga wa Tottenham Erik Lamela, 29, yuko tayari kuondoka klabu hiyo ya London kurejea Italia. Napoli na AC Milan wanamng'ang'ania Muargentina. (Area Napoli, via Team Talk)