Picha ya siku: Kutana na mwanawe Seneta Omanga

Kando na pilka pilka zake za kisiasa, Seneta mteule, Millicent Omanga anajua umuhimu wa kuiweka familia yake mbele ya yote.

Hajawahi iwacha kazi yake ya kisiasa izuie majukumu yake kama mke na mama wa watoto wawili, Wayne na Maya.

Mara kwa mara, Seneta Omanga, huchapisha picha zake na wanawe wakijivinjari nyumbani na kuonesha upendo wake wa mama huku wengi wakitaka kumuiga.

Hii leo, familia ya Omanga inaadhimisha siku ya kuzaliwa kwake Maya na kwa wingi wa furaha na upendo, Omanga alichapisha picha yake katika mtandao wa Insta huku akimsherehekea na kumuombea baraka tele.

"Heri ya siku ya kuzaliwa Maya binti yangu nimpendae. Mungu akuzidishie 🙏. "  Omanga aliandika.

Tazama baadhi ya picha za familia yake ambazo kiongozi huyo ameweza kuchapisha.