LIGI KUU UINGEREZA

Pendekezo la Ek kutaka kuinunua Arsenal lakataliwa

Mashabiki wa Arsenal na Manchester United wamekuwa wakishiriki maandamano dhidi ya wamiliki klabu.

Muhtasari

•Ek ndiye mwazilishi wa huduma ya kimuziki ya Spotify

•Familia ya Kroenke imekataa kuiuza klabu ya Arsenal

Mwanzilishi wa Spotify Daniel Ek
Mwanzilishi wa Spotify Daniel Ek
Image: Hisani

Nia ya mwanzilishi wa huduma ya kusambaza na kuskiza muziki ya Spotify Bw Daniel Ek kutaka kuinunua klabu ya Arsenal imekataliwa.

Kupitia ujumbe wa kuchapishwa, Ek ambaye kwa muda amekuwa akitamani kuinunua klabu hiyo tajika amesema kuwa aliwasilisha pendekezo lake la kununua klabu hiyo kwa mmoja wa wamiliki wa sasa Josh Kroenke na wanabenki wake ila liliangulia patupu.

“Walisema kuwa hawataki pesa zangu na naheshimu uamuzi wao ila bado nina hamu ya kuinunua klabu hiyo iwapo watabadili mawazo” Ek alitangaza.

Ek ambaye alianzisha kampuni hilo la kusambaza muziki la kimataifa mwakani 2006 mjini Stockholm ulio nchi ya Uswidi amekuwa akiunga mkono klabu hicho cha mjini London tangu jadi. Spotify alizinduliwa Kenya mwakani mwezi wa Februari mwakani.

Nia yake ya kuinunua klabu hiyo ilijitokeza baada ya mashabiki kumtaka mmiliki wa klabu hiyo, Stan Kroenke kuiuza baada ya msururu wa matokeo duni. Mashabiki wa Arsenal pamoja na wale wa Manchester United wamekuwa wakishiriki maandamano dhidi ya wamiliki klabu Kroenke na familia ya Glazer ambao wanamiliki Man U.

Ek amependekeza mashabiki kushirkishwa kwenye umiliki na utendakazi wa klabu.