'Ni wakati wa kujivunia kuwakilisha kenya,'Jeremiah anayeshindana katika WRC safari Rally asema

Muhtasari
  • Wakati madereva wa Safari Rally wanaposhindana kila macho yote yatakuwa kwa Jeremiah Wahome wa miaka 22
  • Ni mara ya kwanza kwa dereva Jeremiah kushiriki katika mashindano hayo
Jeremiah Wahome
Image: Twitter

Wakati madereva wa Safari Rally wanaposhindana kila macho yote yatakuwa kwa Jeremiah Wahome wa miaka 22.

Ni mara ya kwanza kwa dereva Jeremiah kushiriki katika mashindano hayo.

Pia ni miongoni mwa orodha ya madereva 58 bora waliowekwa kupigania ushindi katika #WRCSafariRally.

Alianza kupiga karata akiwa na umri wa miaka 8 katika mashindano ya kilabu cha Rift Valley Motorsports. #TwendeTukiuke

Mnamo tarehe 16 Juni Jeremiah alitangaza habari njema kwa wanamitandao kuwa atashiriki katika mashindano hayo.

"Ninafurahi kutangaza kwamba nitashindana katika mashindano ya @wrcsafarirally  yajayo kama mmoja wa madereva wa mpango wa FIA Rally Star

Nitaendesha gari namba 64 Ford Fiesta R3 pamoja na dereva mwenzangu, Victor Okundi katika  natarajia msimu mzuri!" Aliandika Wahome.

Siku ya Alhamisi wakati wa kuanza kwa mashindano hayo kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter alisema kwamba ni wakati wa kujivunia wa kuwakilisha nchi ya kenya katika mashindano hayo.

"Ni wakati wa kujivunia wa kuwakilisha kenya #Naivasha," Wahome aliandika.

Hizi hapa baadhi ya picha za Jeremiah;

Jeremiah Wahome
Image: Twitter