Wanasoka wa Senegal wakasirishwa na marupurupu ya Kombe la Dunia

Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wa zamani na wanamichezo wengine wa Senegal wametilia shaka hatua hiyo.

Muhtasari
  • Mabingwa hao wa Afrika walikuwa wamepewa jukumu la kutinga robo-fainali lakini walitinga katika raundi ya pili

Uamuzi wa Rais Macky Sall wa kukipa kikosi cha soka cha Senegal marupurupu yake ya Kombe la Dunia licha ya timu hiyo kutofikia lengo lake umezua hasira kwa baadhi ya watu katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mabingwa hao wa Afrika walikuwa wamepewa jukumu la kutinga robo-fainali lakini walitinga katika raundi ya pili baada ya kushindwa 3-0 na Uingereza.

‘’Tutalipa kikamilifu marupurupu ya kufuzu kwa robo-fainali kwa ujumbe wote rasmi,’’ Sall alitangaza siku mbili baadaye.

Marupurupu ya Kombe la Dunia - ambayo hutoka kwenye hifadhi ya karibu $23m (£19m) zilizofunguliwa na serikali ya Senegal kulipia gharama za Kombe la Dunia - zitatofautiana kutegemea na ushiriki wa wachezaji 26 katika kampeni nzima, ikiwa ni pamoja na kufuzu.

Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wa zamani na wanamichezo wengine wa Senegal wametilia shaka hatua hiyo.

‘’Ukishinda lazima utazawadiwa, lakini ukishindwa lazima ujifunze kutokana na hilo,’’ mshambuliaji wa zamani wa Simba ya Teranga Diomansy Kamara aliambia gazeti la Stades.

Licha ya tabia yake ya ukarimu, uamuzi wa Sall haukupokelewa vyema na wanariadha kutoka kwa michezo mingine ambao kijadi hulazimika kuchukua juhudi zaidi ili kufadhili ushiriki wao wenyewe katika mashindano.