Mwanariadha Ruth Chepngetich Avunja Rekodi ya Dunia Istanbul

Muhtasari
  • Mwanariadha wa Kenya Ruth Chepng'etich ameweka historia baada ya kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za Istanbul Half Marathon
Ruth chepng'etich
Image: World Athletics

Mwanariadha wa Kenya Ruth Chepng'etich ameweka historia baada ya kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za Istanbul Half Marathon.

Chepng'etich alisajili saa 1:04:02 kushinda mbio hizo mapema Jumapili, Aprili, 4, na kuweka rekodi mpya.

 

Bingwa huyo wa dunia  katika mbio hizo alikabiliana na Hellen Obiri na Muethiopia, Yalemzerf Yehualaw kabla ya kupenya  na kupata ushindi.

Hii ni mara ya tatu Ruth Chepng'etich kunyakua ushindi katika mbio hizo baada ya kuibuka mshindi mwaka 2017 na 2019.

Mwaka 2019, alipambana na Yehualaw katika fainali za mbio hizo kushikilia ushindi wake.