Wataalamu wa ndani ndio wanawasaidia wanariadha wa Kenya kudanganya – Shirika la AIU

Nalyanya na Lempus, walidaiwa kutoa karatasi ghushi kuunga mkono madai yao ya kudungwa sindano ya misuli katika hospitali moja.

Muhtasari

•Kitengo cha Uadilifu wa Riadha kilifikia hitimisho hilo baada ya wanariadha wawili kutumia hadithi sawa kuelezea makosa ya matibabu.

Kenya ni nyumbani kwa wanariadha wanaobobea dunia
Kenya ni nyumbani kwa wanariadha wanaobobea dunia
Image: BBC

Shirika linalosimamia mpango wa kupambana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa wanariadha wa kimataifa limesema kuwa wanariadha wa Kenya wanasaidiwa na wataalam wa matibabu wa nchini humo ili kuficha makosa ya matumizi ya dawa hizo.

Kitengo cha Uadilifu wa Riadha kilifikia hitimisho hilo baada ya wanariadha wawili kutumia hadithi sawa kuelezea makosa ya matibabu.

Wakimbiaji hao, Eglay Nafuna Nalyanya na Betty Lempus, walidaiwa kutoa karatasi ghushi kuunga mkono madai yao ya kudungwa sindano ya misuli katika hospitali moja.

Riadha Kenya ilisema wiki jana kwamba ilikuwa imeahidiwa $5m (£4m) kwa mwaka kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.