Faith Kipyegon na Beatrice Chebet watambuliwa na shirika la kielimu nchini Marekani

Rais Ruto aliwakabidhi wanariadha hao tuzo hiyo ya kifahari

Muhtasari

• Wanariadha wa Kenya Faith Kipyegon na Betarice Chebet wametuzwa tuzo ya kifahari na Chuo cha Mafanikio cha Marekani linalotambua baadhi ya watu wanaofaulu zaidi katika nyanja mbalimbali.

Image: hisani

Wanariadha wa Kenya Faith Kipyegon na Beatrice Chebet wamepokezwa tuzo ya kifahari na shirika la kielimu la Chuo cha Mafanikio cha Marekanini katika hafla iliyoshuhudiwa na rais William Ruto katika jumba la Lincoln Centre Plaza jijini New York.

Chuo cha Mafanikio cha Marekani kinachojulikana kama Academy of Achievements ni shirika la elimu lisilo la faida ambalo linatambua baadhi ya watu wanaofaulu zaidi duniani katika nyanja mbalimbali na kuwapa fursa ya kukutana.

Tuzo ya shirika hilo lilikabidhiwa wanariadha  Faith Kipyegon na Beatrice Chebet kupitia rais William Ruto.

Rais William Ruto amewahongera wanariadha hao akisema kuwa tuzo hiyo ya kifahari itakuwa kumbusho ya kuashiria bidii, talanta na kujitolea kwao katika riadha.

Rais aliongeza kusema kuwa tuzo hiyo itawatia moyo wanariadha wa kesho.

Kwa upande wake waziri wa michezo Kipchumba Murkomen, amewasifia wanariadha hao kwa kusema kuwa dunia nzima imetambua talanta zao, kujitolea kwao kwa riadha na mchango wa athari chanya kwa wanadamu.