Mchezaji kandanda Edison Cavani kuchunguzwa kwa matamshi yake

Muhtasari
  • Mchezaji wa Man United achunguzwa kwa matamshi yake ya ubaguzi wa rangi
  • Edison Cavani alikuwa anamjibu shabiki aliyekuwa anapongeza kwa kuwapa mashetani wekundu ushindi
Image: Hisani

Mechi ya Man United na timu ya Southampton ilisubiriwa sana na mashabiki wa pande zote hasa wa tiu ya Man United jumapili 29 Novemba.

Mchezaji wa Man United Edison aliwasaidia mashetani wekundu kuibuka washindi baada ya mechi hiyo kukamilika kwa magoli 3-2.

Edison Cavani sasa yuko katika uchunguzi baada ya kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram uliosemekana kwamba ulikuwa wa ubaguzi.

Baada ya dakika chahe mchezaji huyo alifuta ujumbe huo baada ya kumjibu shabiki mmoja.

Kulingana na SunSport, shabiki huyo aliandika 'Asi te queiro Matador' katika Kihispania ambalo lina maana kuwa "Ninakupenda, Matador!"

Badala ya mchezaji huyo kumjibu vyema shabiki huyo alitumia matamshi ya ubaguzi wa rangi.

"Gracias Negrito!"ambalo linatafsirika kama ‘Asante Mweusi’. 

Je Cavani atapigwa marufuku baada ya uchunguzi kukamilika na alifanya jambo nzuri? toa maoni yako.