Chelsea wapata kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Arsenal

Muhtasari
  • Chelsea wapata kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Arsenal hii ni baada ya mechi yao ya Desemba 26
  • Arsenal sasa wamo katika nafasi ya 14 huku Chelsea wakishuka hadi kwenye nafasi ya 6

Mechi kati ya Arsenal na timu ya Chelsea ilisubiriwa sana na mashabiki huku wengi wakiwa na matumaini kwamba Chelsea wataibuka washindi bali matumaini yao yalitupiliwa mbali baada ya mechi hiyo kukamilika.

Kikosi cha Arteta kiliingia katika mechi hiyo ya Jumamosi, Disemba 26, kikiwa kinakumbana na msururu wa matokeo mabovu ligini.

Hata hivyo, walijifunga kibwebwe wakati walikuwa wanavaana na Blues na hatimaye kusajili ushindi wao wa kwanza ligini baada ya kujaribu mara nane.

 

Wenyeji walianza kuongoza katika dakika ya 35 kupitia kwa Alexander Lacazette ambaye alichanja mkwaju huo baada ya Reece James kumchezea Kieran Tierney visivyo.

Granit Xhaka, ambaye alikuwa anarejea uwanjani baada ya kulishwa kadi nyekundu katika mechi ya awali, alisawazisha bao hilo dakika moja kabla ya muda wa mapumziko akifaidika na mpira wa bwerere na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Kipindi cha pili kiliwashuhudia Arsenal wakiendeleza mashambulizi yao huku Saka akiweka mwanya kubwa katika mechi hiyo katika dakika ya 56.

Ni hadi dakika ya 85 ndipo vijana wa Frank Lampard walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Tammy Abraham baada ya kumalizia vyema pasi ya Callum Hudson-Odoi.

Jorginho alikuwa na nafasi ya kusawazishia wenyeji wa London magharibi baada ya kupata matuta ya penalti lakini Bernd Leno alipangua kombora lake.

Ushindi huo ulisaidia Arsenal kupanda hadi kwenye nafasi ya 14 na alama 17 jedwalini huku Blues wakishuka hadi nafasi ya sita na pointi 25 nguvu sawa na Aston Villa.