Messi ang'ara katika ushindi wa Argentina dhidi ya Brazil

Muhtasari
  • Messi ang'ara katika ushindi wa Argentina dhidi ya Brazil

Lionel Messi alimaliza kusubiri taji kuu la kwanza la kimataifa wakati Argentina ikiifunga Brazil kwenye fainali ya Copa America kwenye uwanja wa Rio wa Maracana kwa bao moja kwa nunge .

Messi, 34, alianguka chini kwa furaha wakati kipenga cha mwisho kilipopulizwa na alikimbiiwa kwa haraka na wachezaji wenzake, kabla ya kurushwa hewani kwa sherehe, kwani mwishowe alipata heshima ya kiwango cha juu na nchi yake katika mashindano ya 10 muhimu kwake .

Alisaidia pia kumaliza kipindi cha miaka 28 cha Argentina tangu waliposhinda mashindano hayo na aliteuliwa kuwa mchezaji wa mashindano baada ya mabao yake manne kwenye kipute kizima .

Angel di Maria alithibitisha weledi wake kwa kuwafungia bao hilo , baada ya kuchukua pasi ya juu ya Rodrigo de Paul.

Messi alikuwa na nafasi ya kuzidisha ushindi wao lakini aliteleza langoni , katika kile ambacho kingekuwa mwisho mzuri kwa nahodha wa Argentina.

Mabingwa watetezi Brazil walikuwa na mchezo wa kusuasua na nafasi yao pekee ya kukumbukwa ilikuja wakati Richarlison na Gabriel Barbosa walipofanya uokozi kutoka kwa Emi Martinez.

Kinyume na mazuri aliokuwa akipitia Messi mwenzake wa zamani wa Barcelona Neymar alipiga magoti kwa machozi kwenye, wakati harakati zake za kibinafsi za mafanikio ya kimataifa zikiendelea, akiwa amekosa ushindi wa Brazil wa 2019 Copa kupitia jeraha.

Wawili hao, ambao walicheza pamoja Nou Camp kati ya 2013 na 2017 kabla ya Neymar Paris St-Germain, walikumbatiana kwa muda mrefu wakati wakisubiri sherehe ya kupokea kombe

Mchezo ulitazamwa na umati mdogo wa wageni waalikwa 7,000, kwa sababu ya masharti ya Covid-19, lakini ilikuwa ni kwa mara y kwanza shindano kubwa la soka kama hilo kuwa na mashabiki uwanjani

Wafuasi wachache wa nyumbani walitoa sauti zao, ingawa, haswa kila wakati Messi alipogusa mpira,.

Mashindano hayo, yalicheleweshwa kwa mwaka kwa sababu ya janga la corona na kuhamisha kutoka kwa wenyeji wa awali Colombia na Argentina, hadi kwa waandalizi wa 2019 Brazil katika uamuzi wa dakika ya mwisho mwisho ambao ulipokea ukosoaji kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya corona nchini humo .

Imekuwa miaka 15 tangu Messi awakilishe Argentina kwa mara ya kwanza kwenye mashindano makubwa na baada ya mashindano manne ya Kombe la Dunia na mechi sita za Copa America, akicheza mechi 53, mwishowe ana taji kuu la kimataifa yeye - na nchi yake - imetamani kuafikia hilo.

Licha ya kuwa mmoja wa wachezaji bora sana na mahiri wa enzi ya kisasa - na wakati wote - na mataji 10 ya La Liga, manne ya ligi ya Mabingwa na Ballons d'Or sita, maswali juu ya ukosefu wake kung'aa kimataifa yametanda juu yake urithi wake.

Kushindwa mara kwa mara na Argentina limekuwa jambo chungu kwa mshambuliaji huyo, ambaye aliwahi kutangaza kustaafu kwake - kabla ya baadaye kutengua uamuzi huo - baada ya kupoteza fainali ya pili mfululizo ya Copa America mnamo 2016, kushindwa kwake kwa mara ya tatu katika fainali ya mashindano hayo na miaka miwili tu miaka baada ya kushindwa katika fainali ya Kombe la Dunia ya 2014.

Maswali juu ya hatma yake sasa yataendelea kuulizwa, na Messi sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Barcelona kumalizika wiki mbili zilizopita - ingawa Barca wameongeza majaribio yao ya kumshikilia nyota wao na mazungumzo yakiendelea.

Bado kuna matarajio ya Messi kwenda kutumia fursa yake labda ya mwisho kushinda Kombe la Dunia - jambo ambalo Argentina hawajafanya tangu 1986 - ikiwa ataiongoza nchi yake kwenda Qatar akiwa na umri wa miaka 35 mnamo Desemba 2022.