Klabu ya Tottenham Hotspur yamfuta kazi kocha mkuu Nuno

Muhtasari
  • Kwa sasa Spurs inashikilia nafasi ya nane kwenye jedwali la ligi wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea kwa alama 10
Nuno Espirito Santo
Image: Tottenham Hotspur

Klabu ya Tottenham imemfuta kazi kocha wake Nuno Espirito Santo pamoja na timu yake ya ukufunzi ambayo inajumuisha; Ian Cathro, Rui Barbosa na Antonio Dias.

Spurs wamefungwa mechi tano za ligi kuu Uingereza kati ya saba walizocheza ikiwemo ya Jumamosi dhidi ya Manchester United.

 

Kwa sasa Spurs inashikilia nafasi ya nane kwenye jedwali la ligi wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea kwa alama 10

"Najua kwa kiasi gani Nuno na benchi yake ya ufundi walitaka kufanikiwa lakini nasikitika tunalazimika kuchukua uamuzi huu," alisema Mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo Fabio Paratici.

Mwezi Juni mwaka huu, Mreno huyo aliteuliwa kuwa meneja wa Spurs akipewa mkataba wa miaka miwili baada ya kuwa na Wolves kwa miaka minne  .

Tottenham imesema atakayemrithi Nuno "itafahamika hivi karibuni".

Spurs, waliokuwa wanazomewa katika kipigo cha mabao 3-0 nyumbani kutoka kwa United, walianza ligi vizuri wakishinda mechi tatu mfululizo bila kufungwa bao, huku Nuno akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Agosti.