Kwa nini Manchester United haimfuti kazi Ole Gunnar Solskjaer,licha ya matokeo mabaya?

Muhtasari
  • Nahodha wa zamani wa United Gary Neville amesema kuwa matatizo ya United yalikuja kwa haraka
Mkufunzi wa Man United Olegunnar Solskjaer
Image: BBC

Kipigo cha mabao 2-0 kutoka kikosi cha Pep Guardiola, kilijiri chini ya wiki mbili baada ya kile cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool, vimesababisha wengi wakiwemo mashabiki waliokuwa awali wakimuunga mkono Solskjaer, kuamua kuwa raia huyo wa Norway anastahili kufunganya virago.

Licha ya vipigo vipya kutoka kwa mahasimu wao wa jadi na matokeo ya kawaida ambapo wamekusanya pointi nne tu kutoka mechi nne za Ligi Kuu, bado hakuna ishara kutoka Old Trafford kuwa huenda mabadiliko yakatokea.

Hakutakuwepo na shaka kusema kuwa Solskajaer yuko salama ikikumbukwa kuwa likizo ndio wakati klabu huwatimua mameneja. Aston Villa, Norwich na Middlesbrough tayari wamefanya hivyo tangu mechi zao za wikendi zikamilike. Na hivyo kulingana na maoni ya wengi huenda akanusurika.

Suala la kubaki na Solskjaer

Nahodha wa zamani wa United Gary Neville amesema kuwa matatizo ya United yalikuja kwa haraka.

Ni kweli. Licha ya wao kuzoa pointi huko Southampton wakati Cristiano Ronaldo alitikisa wavu mara mbili wakati wa mechi yake ya kwanza tangu arejee katika klabu hiyo dhidi ya Newcstle Septemba 11, Old Trafford ilijawa na furaha nje na ndani ya uwanja

Tangu wakati huo, United wameshinda mechi 4 kati ya 12. Kati ya ushindi huo ule wa Ligi Kuu ulipatikana huko West Ham wakati Mark Noble alikosa penalti ya dakika za lala salama.

Kwenye Ligi ya Mabingwa, Villarreal walikuwa na fursa nzuri huko Old Trafford na Atalanta wakaongoza kwa bao 2-0. Wote walizimwa na mabao ya dakika za mwisho ya Ronaldo. Mreno huyo pia alishiriki kwenye sare dhidi ya Atalanta nchini Italia na kuiweka United kileleni mwa Ligi Kuu zikiwa zimesalia mechi mbili.

United walimpatia Solskjaer kandarasi mpya ya miaka mitatu msimu wa joto baada ya United kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi ya Ulaya. Pia wakampa kandarasi kama hiyo naibu Meneja Mike Phelan, huku mazungumzo yakiendelea ya kuongeza mikataba ya makocha Michael Carrick na Kieran McKeenna.

Uongozi wa klabu ulimtaka Solskjaer kubuni mkakati wa muda mrefu wakihisi kuwa alikuwa bora kufanya kazi hiyo kwani anaielewa klabu.

Tangu Sir Alex Ferguson astaafu mwaka 2013 na sababu kuwa klabu haikuwa imemfuta meneja kwa miongo miwili, United wamejaribu kuweka imani kwa meneja wao wakati kuna changamoto.

Pia wanaelewa kuwa hadhi kinayopewa klabu hiyo inamaanisha kuwa hatua yoyote wakati huu mgumu itazua hisia nyingi.

Iwapo Solskjaer ataondoka kipi kitafuatia?

Kumfuta meneja sio kitu kigumu. Kumpta atakayechukua nafasi yake ndilo suala gumu.

Kutokana na kuwa hakuwa kazini wakati United walipoteza kwa Liverpool na kukubali kureja kutoka Tottenham, ni bayana kuwa Antonio Conte angeajiriwa ikiwa kulikuwa na nia ya kufanya hivyo.

Lakini United haitaki meneja wa mkataba mfupi wa kuajiriwa kwa haraka.

Wanamhitaji meneja ambaye atajenga kikosi na kufanya kazi nao kuwachanganya wachezaji bora zaidi duniani na wale waliofuzu kutoka taasisi za soka.

Mameneja wanaoonekana kuwa na tajriba kama hizo ni pamoja na Mauricio Pochettino, Brendan Rodgers na Erik ten Hag.

Kandarasi yake Pochettino ilongezwa na Paris St-Germain mwezi Julai. Imekuwa kama ni mbinu ya kuzuia ofa kutoka kwa Tottenham na kumpata raia huyo wa Argentina kwa sasa itakuwa changamoto kubwa.

Rodgers amekataa ofa kadhaa tangu alipokuwa na Leicester, lakini alijiunga nao akitokea Celtic katikati ya msimu.

Kocha wa zamani wa Beyern Munich, Ten Hag alikataaa kuhama Ajax kurejea Munich na Hansi Flick akapata kandarasi hiyo mwaka 2019.

Lengo ni lipi?

Baada ya United kunyukwa na Man City, pengo la pointi 11 na viongozi Chelsea lilikuwa kubwa. Lakini baada ya ushindi wa Burnley ambao haukutarajiwa ina maana kuwa kikosi chake Thomas Tuchel sasa wako kipau mbele kwa pointi 9 dhidi ya United baada ya mechi 11.

Ikiwa kulishinda kombe la Ligu Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013 ni lengo katika msimu huu - sawa na vilabu vingine vikubwa pia kuna lengo la kumaliza katika nafasi nne za kwanza na kufuzu kwa mechi za Ligi ya Mabingwa

Kuna ushahidi kuwa viwango vinavyohitajika kufikia hili haviko juu. Kati ya vilabu washindani wa United kwenye nafasi nne za kwanza, West Ham wamepoteza nyumbani dhidi ya Brentford tayari msimu huu, Arsenal majuzi walitoka sare nyumbani na Cystal Palace, United wakaibuka washindi dhidi ya Tottenham na Everton wakapoteza mechi yao ya tatu mfululizo dhidi ya Wolves Novemba mosi.

Mabadilko nafasi za juu

Makamu Mwenyekiti mtendaji Ed Woodward amekuwa akihusika katika utoaji wa maamuzi kwenye klabu hiyo katika kipindi cha miaka 8 sasa,

Hata hivyo baada ya changamoto zilizoikumba klabu, alithibitishwa kuwa ataihama klabu mwishoni mwa mwaka.

Hakuna uhakika kuwa huenda muda ukaruhusu hilo na iwapo Woodward ambaye ni mshirika wa karibu wa familia ya Glazer atabaki kuwa mshauri.

Kuna madai ya ushindani kutoka kwa wengine. Hao ni pamoja na kipa wa zamani wa United Van der Sar, ambaye ana jina zuri kutokana na kazi yake kama mkurugenzi mkuu mtendaji wa Ajax.

Lakini inaonekana kuwa mkurugenzi mtendaji Richard Arnold atachukua nafasi ya Woodward.