Cameroon yawashinikiza wafanyikazi kuhudhuria mechi za Afcon

Muhtasari

•Uamuzi huo umefikiwa baada ya michezo mingi kuchezwa katika mji wa Limbe kukiwa na mashabiki wachache.

Image: ames Copnall

Wafanyakazi wa baraza huko Buea kusini-magharibi mwa Cameroon wanalazimishwa kuhudhuria michezo ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea.

Hii inaambatana na maagizo ya gavana wa mkoa, kulingana na meya wa jiji, ya kutaka watu wote kuhudhuria kwa lazima michezo hiyo.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya michezo mingi kuchezwa katika mji wa Limbe kukiwa na mashabiki wachache.

Buea ni mwenyeji wa timu zinazocheza huko Limbe.

Wakazi wengi wa Buea wanahofia makabiliano kati ya wapiganaji wanaotaka kujitenga na jeshi.

Wapinzani hao walioanza kupigana na serikali takriban miaka mitano iliyopita walikuwa wametishia kuvuruga mashindano hayo lakini serikali imewahakikishia usalama.

Miji kadhaa imetoa mabasi na magari kwa mashabiki wa soka ili kuongeza idadi yao viwanjani.

Serikali ya Cameroon siku ya Juma