Afcon 2021: Kwaheri Ghana, Zimbabwe na Ethiopia

Muhtasari

•Ghana ilimaliza ya mwisho katika kundi C, kwa mshangao wa wengi ambao walikuwa wameipigia mpato kuibuka miongoni mwa mataifa bora katika mashindano ya Afcon 2021.

Image: GETTY IMAGES

Usiku wa Jumanne ulikuwa usiku wa kusahau kwa washindi wa kombe la Afcon mara nne Ghana baada yao kupoteza 2-3 dhidi ya Comoros na kubanduliwa nje ya mashindano hayo.

Ghana ilimaliza ya mwisho katika kundi C, kwa mshangao wa wengi ambao walikuwa wameipigia mpato kuibuka miongoni mwa mataifa bora katika mashindano ya Afcon 2021.

Morocco na Gabon zilimaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia katika kundi C  kwa pointi 7 na 5.

Senegal ilimaliza kileleni mwa kundi B baada ya mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi dhidi ya Malawi kutoka sare ya 0-0. 

Guinea ilichukua nafasi ya pili huku Zimbabwe ikimaliza safari yake ya Afcon 2021 usiku wa Jumanne.

Mnamo Jumatatu Cameroon na Burkina Faso zilihitimu kuingia raundi ya Play Offs baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia. Ethiopia ilibanduliwa nje baada ya kumaliza ya mwisho.