Leeds United yamtimua kocha Marcelo Bielsa

Muhtasari

•Leeds imeandikisha matokeo duni msimu huu huku ikiwa imeshinda mechi tano tu kati ya mechi 26 ambazo zimechezwa tayari.

Marcelo Bielsa
Marcelo Bielsa
Image: HISANI

Klabu ya Premier League Leeds United imempiga kalamu kocha mkuu Marcelo Bielsa kufuatia msururu wa matokeo hafifu.

Mzaliwa huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 66 ameondoka katika klabu hiyo baada ya kuisimamia kwa kipindi cha miaka mitatu unusu.

Hatua hii imejiri masaa machache tu baada ya klabu hiyo ambayo imekalia nafasi ya 16 kwa sasa kupoteza 0-4 ugenini dhidi ya Tottenham.

 

Klabu hiyo inatazamia kufanya kutangaza uteuzi wa kocha mpya hivi karibuni