Kombe la Dunia 2022: Cameroon katika kundi moja na Brazil;Ufaransa na Tunisia

Muhtasari
  • Cameroon katika kundi moja na Brazil;Ufaransa na Tunisia
Image: GETTY IMAGES

Droo ya mechi za kombe la dunia 2022 imetolewa Mechi ya kwanza ya kombe la dunia mwaka huu itakuwa kati ya Qatar dhidi ya Ecuador katika kundi A .

Senegal ipo katika kundi A Pamoja na Qatar, Ecuador, Netherlands huku Tunisia ikijipata katika kundi D Pamoja na France, UAE/Australia/Peru, Denmark.

Morocco ipo katika kundi F Pamoja na Belgium, Canada na Croatia.Cameroon wapo katika kundi G Pamoja na Brazil, Serbia, na Switzerland ilhali Ghana imejipata katika kundi moja na Portugal, Uruguay, South Korea

Droo kamili

Group A: Qatar, Ecuador, Netherlands, Senegal

Group B: England, Iran, USA, Scotland/Wales/Ukraine

Group C: Argentina, Saudi Arabia, Mexico, Poland

Group D: France, UAE/Australia/Peru, Denmark, Tunisia

Group E: Spain, Costa Rica/New Zealand, Germany, Japan

Group F: Belgium, Canada, Morocco, Croatia

Group G: Brazil, Serbia, Switzerland, Cameroon

Group H: Portugal, Ghana, Uruguay, South Korea

Meneja wa England Gareth Southgate, akizungumza na BBC Sport amesema : "Marekani na Iran ni timu ambazo hatujacheza nazo kwa muda mrefu na ya tatu haijulikani lakini inaandaa derby ya Uingereza.

"Lazima tutoke nje ya kikundi. Lengo la kwanza ni kutoka nje ya kikundi na kisha tujenge kutoka hapo.

"Katika hali hii mawazo yetu yote yako kwa watu wa Ukraine, kwa hivyo wakati mechi hiyo inachezwa haina maana.